HOME

Mar 15, 2012

UCHAGUZI MKUU KENYA KUFANYIKA MWAKANI!!

Waziri wa sheria nchini Kenya Mutula Kilonzo


Waziri wa sheria nchini Kenya Mutula Kilonzo amesema kuwa uchaguzi mkuu nchini humo utafanyika mwaka ujao na kuwataka wale wote wanaopinga kukata rufaa mahakamani.


Waziri Kilonzo ameainisha kuwa atalitaka baraza la mawaziri nchini humo kibali cha kufanya mabadiliko ya Katiba ya kupanga tarehe ya uchaguzi mwezi Decemba ya kila mwaka.


Kulingana na katiba mpya uchaguzi mkuu nchini Kenya unatakiwa kufanyika Jumanne ya pili ya kila mwezi Agosti baada ya miaka mitano ambapo Waziri Kilonzo amesema uamuzi wa mahakama ya katiba uko wazi kuwa uchaguzi utafanyika baada ya siku 60 baada ya ukomo wa bunge la sasa.

No comments:

Post a Comment