HOME

Mar 10, 2012

RIHANNA AJITOSA VITA YA JOSEPH KONY!!

Joseph Kony

Mwimbaji nyota duniani Rihanna amewasiliana na shirika la Invisible Children na kuelezea nia yake ya kutaka kushiriki katika mpango wake ulioanzishwa wa kuweka wazi matendo mabaya na kupambana na kiongozi wa waasi wa LRA  Joseph Kony anayesumbua serikali ya Uganda.


Kony ameanza kuandamwa na vyombo mbalimbali duniani sasa kutokana na kampeni hizi zilizoanza, hasa kutokana na kipande cha video kilichowekwa katika mtandaowa You Tube kuonyesha jinsi muasi huyu anavyoiathiri jamii inayomzunguka kwa maovu yake.


Katika video hii, watengenezaji wake pia wanatoa wito kwa watu wengine mashuhuri kuunga mkono kampeni hizi zinazoadhimia kumtokomeza Joseph Kony na kundi lake ambapo msanii Rihanna anakuwa wa kwanza kuonyesha mfano.

No comments:

Post a Comment