Mar 15, 2012
WATATU WAUAWA, WAWILI WAJERUHIWA KWA KUPIGWA NONDO MKOANI MBEYA!!
Watu watatu wamefariki dunia Mkoani Mbeya katika matukio matatu tofauti, likiwemo la mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Daudi Mtereke (26), kuuawa na wananchi wenye hasira kali baada ya kuiba baiskeli kilabuni.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 5:30 usiku huko katika Kijiji cha Nyeregete wilaya ya Mbarali mkoani hapa, ambapo marehemu alifikwa na mauti hayo baada ya kupigwa na wananchi hao, kwa kosa la kuiba baiskeli inayomilikiwa na Bwana Siwajibu Mwihula (22) mkazi wa kijiji hicho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment