Mar 3, 2012
MTANDAO WA WIZI WA PIKIPIKI WABAINIKA TANGA!!
Jeshi la polisi mkoani Tanga limewatia mbaroni watu wawili ambao wameanzisha mtandao wa wizi wa pikipiki katika mikoa ya Tanga na Kilimanjaro na kisha kuanzisha kiwanda cha kuharibu na kisha kuziunda upya kwa ajili ya kuwauzia wafanyabiashara wa usafiri wa bodaboda.
Kamanda wa polisi mkoani tanga Costantine Massawe amesema kuwa kiwanda hicho cha kuziharibu na kuziunda upya pikipiki hizo kimeanzishwa eneo la Duga ambapo pikipiki hizo hizo huundwa na kubandikkwa namba nyingine za usajili pamoja na vifaa vingine vya pikipiki.
Kamanda Massawe amewataja waliotiwa mbaroni kuhusiana na mtandao huo kuwa ni Mtende Mtoo Mausi aliyekamatwa jijini Tanga na mkazi mmoja wa Mnyuzi wilayani Korogwe Abbubakari Twaha aliyekutwa na pikipiki mbili za wizi wilayani humo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment