HOME

Mar 22, 2012

MTUHUMIWA WA MAUAJI UFARANSA AUWAWA!!


Waziri wa mambo ya ndani nchini Ufaransa amesema tukio la polisi kuzingira nyumba katika mji wa Toulouse nchini humo limemalizika huku mtuhumiwa anaedaiwa kufanya mauaji ya watu saba akiwa ameuwawa.


Polisi walivamia nyumba ambayo mtuhumiwa huyo Mohammed Merah  alikuwa ameshikiliwa tangu asubuhi baada ya tukio la kuzingira nyumba hiyo lililodumu kwa takribani saa 32.


Merah alirusha risasi kwa maafisa wa polisi na alikutwa amekufa baada ya kuruka kutoka dirishani ambapo alikuwa akituhumiwa kufanya mauaji ya watu wanne nje ya shule ya Jewish na wanajeshi watatu.


Akizungumza baada ya tukio hilo rais wa Ufaransa Bw. Nicholaus  Sarkozy amevishukuru vikosi vya usalama kwa kazi hiyo kubwa ya kukumbukwa.

No comments:

Post a Comment