HOME

Mar 28, 2012

MTALII AHUKUMIWA NCHINI UGANDA KWA KUWANYANYASA KIJINSIA ZAIDI YA WATOTO 50!!

Emin Baro
Zaidi ya wasichana 50 chini ya umri wa miaka 10 walinyanyaswa kijinsia na mtalii ambaye pia alichukua piacha zao,akawarekodi kwenye mkanda wa video na kuweka picha hizo kwenye mtandao.


Mtalii huyo Emin Baro mwenye miaka 53 ambaye ni mwalimu kutoka Turkey amehukumiwa kifungo cha miaka miwili jela au faini ya shilingi milioni 6 za Uganda na Mahakama ya mwanzo ya Nakawa.


Baro ambaye aliingia nchini humo kama mtalii miaka sita iliyopita amekiri kutenda makosa hayo kwa matumizi mabaya ya kompyuta na kuwa na kumiliki picha za ngono za watoto.

No comments:

Post a Comment