HOME

Mar 22, 2012

WANAJESHI MALI WATANGAZA KUIPINDUA SERIKALI!!





Majeshi nchini Mali yamejitokeza katika kituo cha Televisheni ya taifa ya nchi hiyo kutangaza kuwa yamechukua udhibiti wa serikali saa chache baada ya kushambulia Ikulu ya rais.


Wanajeshi wamesema kuwa hali ya tahadhari nchi nzima imetolewa na kusimamisha katiba ya nchi ambapo majeshi hayo yaliyofanya mapinduzi ya serikali jana yamesema serikali haifanyi jitihada za kutosha za kuwapatia silaha za kupambana na kikundi cha waasi cha kabila la Tuaregs.


Jumuiya ya nchi za Magharibi Ecowas imelaumu hatua hiyo ya majeshi ambapo katika taarifa yake imesema kitendo kilichofanywa na majeshi hayo si cha kiungwana.


Siku ya Jumatano wanajeshi hao walifyatuliana risasi na wanajeshi watiifu kwa serikali.

No comments:

Post a Comment