HOME

Mar 28, 2012

WANAFUNZI CBE WAPEWA ONYO KUVAA NGUO ZISIZO NA MAADILI!!

    
Kaimu mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara Dar es salaam Bw. Athman Ally
















Chuo cha elimu ya biashara cha jijini Dar es Salaam nchini Tanzania (CBE) kimeonya kuwa kitawachukulia hatua kali wanafunzi na watumishi wa chuo hicho watakaovaa mavazi yasiyoendana na maadili ya Kitanzania pamoja na utumishi wa umma.


Kaimu mkuu wa chuo hicho Bw. Athumani Ahmedi amesema kuwa maamuzi hayo yamo katika sheria mwongozo wa mavazi wa chuo hicho ambapo wanafunzi watakaobainika watachukuliwa hatua kali ikiwemo kuzuiwa kuingia chuoni hapo au kusimamishwa masomo kwa kipindi cha miezi mitatu.


Bw. Ahmedi amesema maamuzi hayo magumu yamepitishwa na baraza la utawala la chuo hicho hasa baada ya wanafunzi na watumishi wa chuo hicho kutoheshimu na kukaidi hatua za awali za miongozo ya mavazi ya heshima na yanayoendana na utamaduni wa Kitanzania.

No comments:

Post a Comment