HOME

Mar 28, 2012

KRIS HUMPHRIES AKATAA KUSAINI NYARAKA ZA TALAKA KWA KIM KARDASHIAN!!


Kris Humphries ametoa kali zaidi baada ya kudai kuwa anastahili kulipwa dola 97,222, zaidi ya shilingi milioni 155 za kitanzania kila siku ndani ya muda wa siku 72 ambao ndoa yake na Kim Kardashian ilidumu ikiwa ni katika taratibu za kukamilisha masuala ua talaka.


Kris anawekea vikwazo mbalimbali katika taratibu za makubaliano ya kuachana kwake na Kim kwa kukataa kusaini nyaraka za talaka mbali na kuwa zimezingatia malipo mazuri ya kuvunja mkataba huo, lakini kwa hesabu za jumla, jamaa huyu anataka dola milioni 7, zaidi ya shilingi bilioni 11 za kitanzania.


Kim anashukiwa kujiingiza katika ndoa na Kris ili kujipatia faida kibiashara na jambo hili limemuumiza sana Kris ambaye kwa sasa anakomaa kwa kuamini kuwa pengine kuongeza muda zaidi wa kushughulikia talaka yake kutampatia fursa ya kuvuna pesa zaidi.


Hata hivyo Mwanadada Kim amesisitiza kuwa alifunga ndoa na Kriss kutokana na Upendo na sio kwa malengo ya kujipatia faida kama inavyotafsiriwa

No comments:

Post a Comment