HOME

Mar 27, 2012

KENYA YAFANYA MABADILIKO MAKUBWA BARAZA LA MAWAZIRI!!

Waziri mpya wa sheria Eugene Wamalwa (kulia) akikabidhiwa ofisi na Mhe. Mutula Kilonzo aliyekuwa waziri wa wizara hiyo.
Waziri mpya wa sheria nchini Kenya aliyeteuliwa katika mabadiliko ya baraza la mawaziri Eugene Wamalwa ambaye ni mbunge wa jimbo la Saboti amesema kwamba atatekeleza katiba mpya na kutumikia kwa uwezo wake wote kitaaluma.


Mabadiliko hayo makubwa ya baraza la mawaziri yamepelekea waziri wa utalii wa nchi hiyo Bw. Najib Balala kufukuzwa.


Mawaziri Moses Wetangula na Mutula Kilonzo wamehamishwa katika mabadiliko hayo makubwa yaliyotangazwa jana usiku na rais Mwai Kibaki na waziri mkuu Raila Odinga.


Waziri Wetangula ambaye amerejea nchini humo Jumapili usiku baada ya kukwama nchini Mali kufuatia mapinduzi ya Serikali amehamishiwa wizara ya biashara wakati Mutula Kilonzo amekuwa mkuu wa wizara ya elimu akichukua nafasi ya Bw. Sam Ongeri ambaye amekuwa waziri wa mambo ya nje.


Waziri mpya wa sheria nchini Kenya aliyeteuliwa jana Eugene Wamalwa amesema kwamba atatekeleza katiba mpya na kutumikia kwa uwezo wake wote kitaaluma.

No comments:

Post a Comment