HOME

Mar 27, 2012

ALIYEMKASHIFU MUAMBA KWENDA JELA!!

Liam Stacey,akiwasili mahakamani.
Mahakama ya Uingereza imemhukumu kwenda jela mwanafunzi aliyeweka ujumbe wa kibaguzi uliomkejeli Fabrice Muamba katika mtandao wa Twitter ambapo mcheza soka huyo alizirahi baada ya moyo wake kusimama wakati akichezea klabu yake mapema mwezi huu.


Liam Stacey mwenye umri wa miaka 21 amekiri kuchochea chuki za ubaguzi wa rangi ambapo amepelekwa jela siku 56.


Muamba amepata nafuu japo yupo katika chumba cha wagonjwa mahututi ambapio mechi kati ya klabu yake ya Bolton na Tottenham michunao ya FA ambao ulisimamishwa baada yake kuzirahi unachezwa tena leo usiku.

No comments:

Post a Comment