Mar 7, 2012
23 WAFA AJALINI UGANDA!!
Watu 23 wamethibitika kufariki dunia nchini Uganda na wengine wengi kujeruhiwa baada ya gari la mizigo ambalo walikuwa wanasafiria kutumbukia ndani ya mto katika wilaya ya Arua jana jioni.
Msemaji wa jeshi la polisi huko Nile magharibi Josephine Angucia amekaririwa akisema leo asubuhi kuwa bado zoezi la kuitoa miili ya marehemu kutoka kwemye mto huo inaendelea.
Polisi imesema miili 18 imekwishatolewa ndani ya mto huo na kupelekwa katika hospitali za Arua na Kuluva huku kukiwa na hofu kuwa baadhi ya miili itakuwa imekwama ndani ya mabaki ya gari hilo mtoni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment