HOME

Mar 10, 2012

MGOGORO WA KIUCHUMI HUENDA UKAMALIZIKA BARANI ULAYA!!

Mkurugenzi wa shirika la fedha duniani IMF, Christine Lagarde

Mkurugenzi wa shirika la fedha duniani IMF, Christine Lagarde amesema kuwa kwasasa mdororo wa kiuchumi kwenye ukanda wa Jumuiya ya Ulaya huenda ukapata suluhisho na kumalizika kabisa.


 Lagarde ameyasema hayo kufuatia hapo jana wakopeshaji binafsi nchini Ugiriki kuipatia mkopo nchini ya Ugiriki ambayo sasa kuna uwezekano mkubwa nchi hiyo kuondokana na matatizo ya kiuchumi.


Siku ya Alhamisi ilikuwa siku ya mwisho kwa wakopeshaji binafsi kuhakikisha wanaipatia Ugiriki mkopo miwngine wa fedha, mpango ambao awali wakopeshaji hao walitishia kusogeza muda mbele kwakile walichoeleza kuwa ni wasiwasi wa serikali hiyo kutumia mkopo huo.


Kiongozi huyo amesema kuwa kwa hali inavyoonekana hivi sasa, ni wazi kuwa nchi ya Ugiriki itaondokana na madeni makubwa ambayo yanaikabili na kwamba matatizo ya kicuhumi yatapatiwa ufumbuzi kutokana na mkopo ambao wamepatiwa.

No comments:

Post a Comment