Dk Joyce Ndalichako |
Baraza la Mtihani la Tanzania (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya kidato cha sita iliyofanyika Februari mwaka huu yakionyesha kuongezeka kidogo kwa kiwango cha ufaulu kwa ujumla huku wavulana waliofaulu wakiwaacha mbali wasichana.
Katika matokeo hayo yaliyotangazwa jana na Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Joyce Ndalichako, kati ya watahiniwa 46,499 waliofanya mtihani huo, wavulana waliofaulu ni 30,466 wakati wasichana ni 16,033. Hata hivyo, kumekuwa na mchuano mkali katika ufaulu kwa asilimia ambao wasichana walipata 87.37 na wavulana 87.69.
Sekondari ya Wasichana ya Marian, Bagamoyo ndiyo iliyoongoza kitaifa na mwanafunzi wake, Faith Assenga ndiye aliyeshika namba moja katika masomo ya Sayansi.
“Katika masomo ya Biashara, aliyeshika nafasi ya kwanza ni Alex Isdor wa Sekondari ya Kibaha na Lugha ni Faridi Abdallah wa Sekondari ya Mpwapwa,” alisema Dk Ndalichako.
Dk Ndalichako alisema kiwango cha kufaulu kwa watahiniwa 46,499; wakiwemo wale wa kujitegemea, kimeongezeka kutoka asilimia 87.24 mwaka jana hadi 87.58 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment