HOME

May 5, 2012

TAHADHARI YA KUTOTEMBEA USIKU YATANGAZWA MISRI!!

Amri ya kutotembea ovyo usiku imetangazwa nchini Misri, katika eneo linalozunguka wizara ya ulinzi mjini Cairo kufuatia mapigano yaliyozuka kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama hapo jana.

Ghasia hizo zilizuka baada ya waandamanaji kupuuza onyo la jeshi la kutokaribia eneo la wizara hiyo ya ulinzi na kuanza kulishambulia jengo la wizara hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa ya serikali, mwanajeshi mmoja ameaga dunia kutokana na majeraha huku mamia ya watu wakiwa wamejeruhiwa.

Waandamanaji kadha wamekamatwa na maafisa wa ulinzi na kwa sasa wanazuiliwa katika vituo mbali mbali vya kijeshi.

No comments:

Post a Comment