Rapa na muigizaji mkongwe - Queen Latifah anatarajiwa kuongoza tamasha kubwa kabisa la LGBT ambalo limekuwa likitazamwa tofauti na maelfu ya watu, na Queen atapanda jukwaani kwaajili ya kuburudisha idadi kubwa ya mashabiki wanaotarajiwa kuhudhuria.
LGBT inasimama badala ya Long Beach Lesbian and Gay Pride Festival, tamasha ambalo linawakutanisha wapenzi wa jinsia moja kutoka sehemu mbalimbali, na kwa kuongoza tamasha kama hili, Queen Latifah anaweka rekodi ya kuwa mtu mashuhuri wa kwanza kuwa na moyo wa kuongoza kitu kama hiki.
Kutoka katika jamii ya hip hop, r&b, hadi pop, Queen Latifah ana simama kama sauti ya kizazi cha sasa na tamasha lake litakuwa ni la aina ya kipekee, alisikika akisema mmoja wa kiongozi wa tamasha la Long Beach Pride - Pat Crosby.
No comments:
Post a Comment