Milipuko miwili imepiga katika mji mkuu wa Syria Damascus huku kituo cha Televisheni cha nchi hiyo kikisema kuwa mamia ya watu wameuwawa na wengine kujeruhiwa katika shambulio hilo la kigaidi.
Katika picha za video za mlipuko zimeonyesha uharibifu mkubwa katika kitongoji cha al-Qazzaz kusini mwa mji wa Damascus.
Mji huo umekuwa ukilengwa na mashambulio kadhaa ya mabomu katika miezi ya hivi karibuni kufuatia mgogoro wa kupinga serikali yua nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment