Mfuko wa taifa wa bima ya afya nchini Kenya NHIF jana uliingia katika tukio lililofananishwa na mchezo wa kuigiza, baada ya mwenyekiti wa mfuko huo kuifukuza bodi ya mfuko huo, bodi kurudishwa madarakani na waziri wa huduma afya dakika chache baadae, kisha mtendaji huyo kufukuzwa na waziri.
Katika tukio hilo lilioshuhudiwa na watu hadharani wakiwemo waandishi wa habari , mwenyekiti wa mfuko huo Richard Muga alitangaza kuwasimamisha kazi mameneja watano, akiwemo mtendaji mkuu,Bw. Richard Kerich.
Hata hivyo, Waziri wa huduma za afya, Anyang’ Nyong’o, waliwarudhishaamaeneja hao madarakani mara moja, kisha akamsimamisha kazi mwenyekiti huyo papo hapo.
No comments:
Post a Comment