Aliyekuwa mshiriki wa shindano la Big Brother ambaye pia ni balozi wa vita dhidi ya Malaria kutoka nchini Kenya Sheila Kwamboka amesema kuwa katika siku za usoni anatarajia kujiingiza katika fani ya uigizaji.
Sheila hakuweka wazi zaidi kuhusiana na aina ya uigizaji ambao atakuwa anaufanya, na itakuwa ni katika mpango gani, lakini mwanadada huyu amewataka mashabiki wake kutarajia kumuona akitokea katika televisheni hivi karibuni.
Sheila pia amesema kuwa amekwisharekodi nyimbo kadhaa pamoja na wasanii wakali wa muziki kutoka Kenya, lakini kwake yeye bado ni mapema mno kuwataja kwa kuwa kazi hizi ni za ushirikiano na yeye hataki kuwa msemaji wake mpaka pale zitakapotoka
Kwa sasa Sheila kupitia shirika lake la hisani la Sauti Za Africa, wapo katika mpango wa kutengeneza makala kwaajili ya kuelimisha zaidi watu juu ya ugonjwa huu.
No comments:
Post a Comment