Megrahi alihamishwa kutoka gereza la Scotland mwaka 2009 akiwa anaugua saratani |
Maziko ya Mtu aliyeshtakiwa kwa kuilipua ndege kwa mabomu Lockerbie mwaka 1988 Abdelbaset al-Megrahi ambaye amefariki dunia nyumbani kwake Tripoli jana yamefanyika nyumbani kwao huko Tripoli.
Megrahi ni mtu pekee aliyeshtakiwa kwa kulipua ndege hiyo iliyosababisha vifo vya takribani watu 270 ambapo alishtakiwa na mahakama maalum huko Uholanza mwaka 2001.
Megrahi alihamishwa kutoka gereza la Scotland mwaka 2009 akiwa anaugua saratani ambapo waziri mkuu wa Uingereza Bw. David Cameroon amesema ni siku ya kukumbuka wahanga 270 waliokufa katika tukio hilo kubwa la kigaidi.
No comments:
Post a Comment