HOME

May 3, 2012

ODINGA AMPA UHURU MUDAVADI KUHAMA!!

Waziri Mkuu wa Kenya Raila Odinga amejibu hatua ya naibu wake Musalia Mudavadi kukihama chama cha Orange Democratic Movement (ODM) na kusema alikuwa huru kuchukua uamuzi wake.

Odinga amesema kama kiongozi anayetetea demokrasia, hawezi kushtumu uamuzi wa naibu wake ambaye amejiuzulu pia kama waziri wa serikali za mitaa.

Aidha Odinga ambaye ni kiongozi mkuu wa chama cha ODM amesema ataachia baraza kuu la chama kuamua ikiwa itamuondoa kwenye chama Mudavadi na hivyo kupoteza kiti chake cha ubunge hatua ambayo huenda ikamfanya Naibu Waziri Mkuu kurudi kwenye uchaguzi katika jimbo lake la Sabatia, Magharibi mwa Kenya.

No comments:

Post a Comment