Kampuni ya mawasiliano kwa njia ya mtandao wa intaneti ya Facebook, imetangaza bei ya hisa zake inazotarajia kuziuza hivi karibuni, kwa bei ya kati ya dola za Marekani 28 na 35 kwa kila hisa moja.
Hisa hizo zitaanza kuuzwa kwa kutumia nembo ya FB, na kufanya thamani halisi ya kampuni hiyo kufikia dola za Marekani bilioni 95.
Mauzo hayo ya hisa ni makubwa kuwahi kufikiwa na kampuni za biashara za mtandao, kiasi cha kuizidi kampuni ya Google ambayo mwaka 2004 iliuza hisa zenye thamani ya dola za Marekani bilioni 23..
No comments:
Post a Comment