Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Jakaya Kikwete leo amefanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri ambapo mawaziri kadhaa wamepoteza nafasi zao.
Katiba baraza hilo jipya alilolitangaza leo Ikulu Jijini Dar es Salaam Rais Kikwete pia amefanya mabadiliko ya mawaziri pamoja na manaibu ikiwa ni katika kile kilichoelezwa kuwa ni kulisuka upya baraza la mawaziri.
Miongoni mwa mawaziri waliopoteza Uwaziri wao ni pamoja na Waziri wa Fedha Mh. Mustafa Mkulo, Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngeleja, Waziri wa Maliasili na Utalii Mh. Ezekiel Maige, Waziri wa Uchukuzi Omary Nundu, Waziri wa Afya Dk. Haji Mponda pamoja na Waziri wa Viwanda na Biashara Cyril Chami.
No comments:
Post a Comment