Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor leo amehukumiwa kifungo cha miaka 50 jela baada ya mwezi uliopita kutiwa hatiani kwa makosa ya uhalifu wa kivita na mahakama maalumu ya Umoja wa Mataifa huko The Hague hukumu iliyotolewa na Jaji Richard Lussick.
Waendesha mashtaka wa mahakama maalumu ya Sierra Leone waliitaka mahakama hiyo kumfunga mtuhumiwa huyo miaka 80 jela ambapo upande wa utetezi ulidai kuwa adhabu hiyo ni kubwa mno.
Taylor amesisitiza kuwa hana hatia na anatarajia kukata rufaa kupinga adhabu hiyo na mchakato wa rufaa unaweza kuchukua zaidi ya miezi sita.
Mahakama hiyo ilimtia hatiani Taylor kwa mashitaka 11 yanayohusiana na uhalifu wa kivita, ubakaji na mauaji.
No comments:
Post a Comment