HOME

May 5, 2012

MKURUGENZI MKUU WA BODI YA NHIF KENYA NA MAAFISA WAKE WATIMULIWA KAZI!!

Francis Kimemia
Kaimu mkuu wa utumishi wa umma nchini Kenya Francis Kimemia amewatimua kazi maafisa wa bodi nzima ya mfuko wa bima ya afya NHIF ikiwa ni pamoja na mkurugenzi mkuu wa bodi hiyo.


Katika taarifa yake Kimemia amesema serikali itaiteua bodi ya uangalizi wa utawala na kuanzisha uchunguzi wa madai ya rushwa yaliyotawala katika mpango mzima wa utoaji huduma za matibabu kwa watumishi wa umma.


Amesema hatua hiyo ni kulinda maslahi ya umma katika taaissisi hiyo kufuatia madai yaliyoripotiwa kwa kiasi kikubwa na vyombo vyote vya habari vikiwemo radio,televisheni pamoja na magazeti.

No comments:

Post a Comment