HOME

May 4, 2012

AKAUNTI YA SIMU YA KUMCHANGIA SAJUKI YACHAKACHULIWA!!

Sajuki akiwa na mkewe Wastara siku walipofunga ndoa.

Harakati mbalimbali zinaendelea kwa ajili ya kumchangia fedha za matibabu msanii wa maarufu katika tasnia ya filamu nchini Tanzania Juma Kilowoko maarufu kama Sajuki ambaye anasumbuliwa na uvimbe tumboni ili aweze kwenda India kutibiwa lakini wanaojiita wajanja wa mjini wameingilia mchakato huo mzima na kuamua kuchakachua akaunti ya Tigo pesa inayotumika kuchangia.

Kwa mujibu wa mmoja wa waigizaji ambao wako bega kwa bega na familia ya Sajuki Dinno kuna watu wanaichakachua akaunti hiyo na kutoa pesa juu kwa juu na kisha kuiblock na kuitupa line ya simu lakini wao baada kugundua mchezo huo wamewasiliana na meneja wa mtandao huo ambaye ameifunga kwa muda namba hiyo ili kuishughulikia.

Dinno amesema mpaka sasa ndio wanajaribu kufuatilia kujua ni kiasi gani kimeibwa wapo katika harakati pia za kufanya mahesabu baada ya kufanya zoezi la kuchangia kujua wamepata kiasi gani na bado shilingi ngapi huku wakifanya mipango ya safari ya mgonjwa anayetegemewa kusafiri wiki ijayo na Bado unaweza kuchangia kwa Mpesa 0762 189 592 na kupitia Akiba commercial bank acount no 050000003047 Wastara Juma.

No comments:

Post a Comment