Mbunge wa jimbo la Mwea Peter Gitau |
Mwanamke raia wa Kenya anaedai kuwa ana mtoto wa miezi miwili aliyezaa na mbunge amedai shilingi za Kenya milioni 1.2 kutoka kwa mbunge huyo kwa ajili ya matunzo ya mtoto.
Hata hivyo mbunge huyo wa jimbo la Mwea Bw. Peter Gitau amekana madai hayo akisema ameoa na ana familia yenye furaha.
Katika kesi hiyo iliyofunguliwa katika mahakama jijini Nairobi mwanamama huyo mwenye umri wa 21 anayefanya kazi katika kampuni binafsi amedai kuwa mbunge Gitau alimpa ujauzito na kisha kumtelekeza.
Ameendelea kudai kuwa mbunge huyo alimuahidi kumpatia kazi, gari na nyumba iwapo atamzalia mtoto.
No comments:
Post a Comment