HOME

May 9, 2012

TANZANIA YATOA MSIMAMO WAKE JUU YA MGOGORO WA MOROCCO NA SAHARA MAGHARIBI!!

Waziri wa mabo ya nje wa Tanzania Mhe. Bernard Membe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo.
Nchi za Afrika zimetakiwa kuwa makini dhidi ya tishio jipya ya mgawanyo wa bara la Afrika kutokana na uchu wa mataifa ya kigeni, dhidi ya rasilimali za bara hilo kama ilivyofanywa na wakoloni huko jijini Berlin Ujerumani mwaka 1884.

Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania,Bernard Membe amesema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati akielezea msimamo wa Tanzania kuhusu harakati za Sahara Magharibi za kutaka kutambuliwa kama taifa huru nje ya utawala wa Morocco.

Kwa mujibu wa waziri Membe, nchi za Ulaya, Asia na Amerika zimekuwa zikifanya harakati ya kuchukua rasilimali na kujenga mtandao wa masoko ya bidhaa zao barani Afrika, kupitia mikataba ya isiyo na maslahi kwa Waafrika wenyewe.

Amewataka viongozi wa Afrika kutumia mkutano wa kimataifa wa uchumu unaoendelea jijini Addis Abbaba Ethiopia, kufikia maazimio yatakayohakikisha ulinzi wa rasilimali za Afrika dhidi ya tishio hilo.

No comments:

Post a Comment