Rais wa Afrika Kusini Bw. Jacob Zuma amesema Mzee Nelson Mandela atahamia katika makazi yake ya tangu utotoni katika kijiji cha Qunu na kuongeza kuwa mwasisi huyo wa taifa yupo katika afya njema.
Mandela amekuwa akiishi nyumbani kwake jijini Johannesburg wakati makazi ya kijiji cha Qunu, yaliyopo Mashariki mwa jimbo la Capetown yamekuwa yakifanyiwa ukarabati.
Msemaji wa rais Bw. Mac Maharaj amekaririwa na shirika la habari la
SAPA akisema kuwa mzee Mandela ameonyesha nia yake ya kutaka kurejea kijiji cha Qunu ambacho amekulia.
No comments:
Post a Comment