HOME

May 7, 2012

CAG AWAONYA MAWAZIRI WAPYA!!

CAG Ludovick Utouh
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amewaonya mawaziri wapya na watendaji serikalini kwamba ripoti zake hivi sasa zina nguvu za kusimamia uwajibikaji hivyo, wanapaswa kusimamia vyema wizara zao kuzuia ubadhirifu wa fedha za umma.

Kauli hiyo ya Utouh ni ya kwanza tangu ripoti yake ya mwaka huu kuwang’oa mawaziri sita kati ya wanane ambao wizara zao zilionekana kugubikwa na ufisadi wa fedha za umma.

Akizungumza jana, Utouh alisema mawaziri wanapaswa kufahamu kwamba kuanzia sasa hadi mwaka 2015, zitatoka ripoti nyingine tatu, hivyo ni vyema wakachukua tahadhari wakiwa ndiyo wasimamizi wakuu wa shughuli za wizara.

Alisema kilichotokea bungeni na hadi mawaziri kuwajibishwa, kimethibitisha kuwa sasa kutakuwa na uwajibikaji mkubwa utakaosababishwa na ripoti zake kama watendaji wasipofuata taratibu za Serikali.

No comments:

Post a Comment