Watu tisa wamekufa katika mafuriko yaliyoendelea kukumba maeneo mbalimbali ya Kenya kufuatia mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini humo.
Kati ya waliokufa ni watu wanne ambao walisombwa na mafuriko katika vitongoji vya Ongata Rongai ambapo miili kyao ilipatikana leo asubuhi juu ya daraja la Rimpa huko Longai.
Huko Kiseria gari lililokuwa na watu wawili ndani yake lilisombwa na maji huku jitihada za kuokoa miili yao zikiendelea wakati mwanaume mmoja amezama wakati akivuka mto Acacia.
No comments:
Post a Comment