Mtuhumiwa Bw. Swalehe Mshana akiwa chini ya ulinzi mkali |
Ofisi ya Afisa mtendaji wa kata ya Kinondoni jijini Dar es salaam imemtia mbaroni mmoja wa watu wanaodaiwa kuwa ni matapeli kwa kusema wao ni mabwana afya na hatimaye kuchukua fedha kwa njia za udanganyifu kutoka kwa wananchi.
Mtuhumiwa huyo Bw. Swalehe Mshana mkazi wa jiji la Dar es salaam alikamatwa na kufungwa pingu na kufikishwa katika ofisi za kata ya Kinondoni ambapo amekuwa akijifanya bwana afya na kuwakagua watu na kisha kuwachukulia fedha.
No comments:
Post a Comment