Mamlaka katika mji wa Dusa Mareb nchini Somalia zimesema takribani watu saba wakiwemo wabunge wawili wameuwawa katika shambulio la bomu katikati ya nchi hiyo.
Mashuhuda wa tukio hilo wameliambia shirika la habari la BBC kuwa shambulio hilo lilikuwa limelenga kikundi cha wanasiasa 20 waliokuwa katika mgahawa wa wazi.
Wanasiasa hao walikuwa wamesafiri kwenda mji wa Dusa Mareb uliopo Galgadud unaodhibitiwa na majeshi yanayounga mkono serikali ya nchi hiyo kuhamasisha mapatano.
Kikundi cha kiislamu cha Al-Shabaab kimesema kimehusika na shambulio hilo.
No comments:
Post a Comment