HOME

May 5, 2012

MKUU WA WILAYA YA MBOZI MKOANI MBEYA AJIUZULU!!

Mkuu wa wilaya ya Mbozi mkoani Bw. Gabriel Kimolo ametangaza kujiuzulu wadhifa wake kuanzia na kutoa baada ya sababu kwamba ni ubabaishaji wa baadhi ya watendaji walioko serikalini ambao wanakwamisha maendeleo katika wilaya ya Mbozi.


Akizungumza katika kikao maalumu na waandishi wa habari Jijini Mbeya Kimolo amesema kuwa dhamira yake imemsukuma kuamua kuachia wadhifa huo kwa hiari na kwamba anajikita katika shughuli zake binafsi.


Amesema kuwa kwa kipindi kirefu amekuwa akifanya kazi katika mazingira magumu huku akizongwa na baadhi ya wafanyabiashara wa kahawa ambao wamekuwa na kiburi cha kununua kahawa mbichi kinyume cha tamko la serikali ya mkoa hali ambayo imemfanya ashindwe kutimiza majukumu yake kama Mkuu wa Wilaya.


Pia amesema kuwa uteuzi wake wa Mkuu wa Wilaya ya Mbozi ulianza mwaka 2006 na kukoma mwaka 2010 na kwamba baada ya hapo amekuwa akishindwa kujiwekea mipango na mikakati ya uendeshaji wa wilaya kutokana na kucheleweshwa kutangazwa katika awamu nyingine ya uongozi.


Amesema uteuzi mwingine wa kipindi cha 2011 hadi 2015 kama ilivyo sheria ya mkataba wa uteuzi wangu sasa ni kipindi cha mwaka mmoja na nusu, kipindi ambacho amedai kwamba kimemwathiri katika utendaji kikazi kama mkuu wa wilaya na familia yake kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment