Siku tatu za maombolezo ya kitaifa zimetangazwa kuanzia leo nchini Nigeria kufuatia ajali ya ndege ambapo zaidi ya 150 walikufa.
Ndege hiyo aina ya Boeing MD-83 iliangukia eneo moja la kuchapisha karatasi na makaazi mjini Lagos kabla ya kulipuka. Makundi ya wokozi yamekuwa eneo la ajali usiku kucha.
Taarifa zinasema abiria wote katika ndege hiyo walikufa. Hakuna majeruhi katika eneo la ajali japo haijabainika rasmi ni watu wangapi ambao wamekufa.
Ndege hiyo inamilikiwa na kampuni ya Dana Air ambayo hutoa huduma zake kati ya mji wa Abuja na Lagos. Ajali hiyo ilitokea katika mji wa Iju Kaskazini mwa uwanja wa ndege.
No comments:
Post a Comment