HOME

May 30, 2012

MZEE MANDELA KUREJEA KUISHI KIJIJI ALICHOKULIA!!

Rais wa Afrika Kusini Bw. Jacob Zuma amesema Mzee Nelson Mandela atahamia katika makazi yake ya tangu utotoni katika kijiji cha Qunu na kuongeza kuwa mwasisi huyo wa taifa yupo katika afya njema.

Mandela amekuwa akiishi nyumbani kwake jijini  Johannesburg wakati makazi ya kijiji cha  Qunu, yaliyopo Mashariki mwa jimbo la Capetown yamekuwa yakifanyiwa ukarabati.

Msemaji wa rais Bw. Mac Maharaj amekaririwa na shirika la habari la
SAPA akisema kuwa mzee Mandela ameonyesha nia yake ya kutaka kurejea kijiji cha Qunu ambacho amekulia.

MARK ZUCKERBERG AISHIWA??

Mwasisi wa Facebook Mark Zuckerberg alihitaji kuchaji mfuko wake huko Italy kwa kusimama katika moja ya ATM katika kisiwa cha Capri baada ya kupoteza takribani dola bilioni 1.5 katika saa chache tu.

DAR KUZIZIMA JUMAMOSI HII KATIKA TAMASHA LA KTMA WINNERS TOUR CONCERT!!

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro George Kavishe akizungumza jijini Dar es salaam leo.
Tamasha la washindi wa tunzo za muziki Tanzania, zijulikanazo kwa jina la Kilimanjaro Tanzania Music Awards Winner’s Tour kwa mwaka huu zinafikia ukingoni Jumamosi hii ya tarehe 02 Juni, katika viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

Huu utakuwa ni mkoa wa sita kufanyika tamasha hili kubwa  na zuri ambalo lina dhana kuu tatu ambazo ni kwanza kutoa burudani kwa wapenzi wa bia ya Kilimanjaro Premium Lager ambao ndio wadhanimini wakuu wa mchakato mzima, Dhana ya pili ni kuwapa wasanii walioshinda tunzo nafasi ya kuonana na mashabiki wao na kuwashukuru kwa kushiriki vilivyo zoezi la upigaji kura na kuwawezesha kuwa washindi wa tunzo hizi kubwa na za kipekee katika ukanda wa Afrika ya Mashariki na Kusini mwa jangwa la Sahara. Na dhana ya tatu, ni kuwathibitishia mashabiki wao hao hao kwamba hawakubahatisha kupewa tunzo hizi, kwa kufanya onesho zuri litakaloacha msisimko wa mwaka mzima kutokana na ukubwa wake, na pia kwa kuzingatia kwamba wasanii wanaoshiriki tamasha hili ni wale ambao ni bora kabisa kwa kipindi hiki na ndio sababu wakatunukiwa tunzo.

Kabla ya Tamasha hili kubwa la Dar es Salaam, wasanii hawa wamepita takriban mikoa mitano huku shughuli za Tamasha zikiambatana na zoezi la kutafuta vipaji ambalo limefanikiwa kuibua vipaji sita ambavyo vitaonekana siku ya tamasha.

Mikoa ambayo Tamasha limepita ni mikoa ya Dodoma, Mwanza, Moshi, Mbeya na Mtwara ambapo kila mkoa ulitoa mshiriki mmoja chipukizi katika zoezi jipya la kutafuta vipaji lililopewa jina la Kilimanjaro Awards Talents Search, isipokuwa Dodoma tu iliyotoa washiriki wawili ambao walilingana alama.

Zoezi hilo lenye lengo la kuibua vipaji vya mikoani lilisimamiwa na Majaji wanne ambao ni Mshindi wa tunzo ya wimbo bora wa Reggae Queen Darleen, wanamuziki wakongwe wa muziki wa Bongoflava Profesa Jay na Juma Nature pamoja na Henry Mdimu, ambaye ni Mhariri wa Burudani wa kampuni ya Mwananchi Communications Limited.

Kutoka Dodoma, chipukizi waliopatikana, ambao watashiriki kwenye tamasha hili kubwa na la aina yake ni Issa Dubat na Juma Madaraka, kutoka Mbeya ni neema, kutoka Mwanza ni Christina, kutoka Moshi ni Sungura na kutoka Mtwara ni Nicolaus. Hawa ndio chipukizi kutoka mkoani ambao watafungua tamasha hili na kufuatiwa na washindi wa tunzo za Kili Mwaka huu ambao kwa idadi, watakuwa 14 kwa jumla.

Wasanii hao ni Diamond ambaye anashikilia tunzo tatu, Ommy Dimpoz ambaye ni msanii bora anayechipukia ambaye pia anashikilia tunzo ya wimbo bora wa AfroPop, Ally Kiba ambaye ni mtumbuizaji bora wa kiume, na Barnabas Elias ambaye ni msanii bora wa kiume kwa mujibu wa tunzo za Kilimanjaro za mwaka huu.

Wengine watakaopanda jukwaani ni pamoja na Roma Mkatoliki ambaye anashikilia tunzo ya mwanamuziki Bora wa Hip Hop ambaye pia amenyakua tunzo ya wimbo bora wa Hip Hop, Isha mashauzi ambaye amenyakua tunzo ya wimbo bora wa taarab, Suma Lee ambaye anashikilia tunzo ya wimbo bora wa mwaka, Queen Darleen, Kitokololo ambaye anashikilia tunzo ya rapa bora wa bendi, na AT ambaye ana tunzo ya wimbo bora wenye asili ya kitanzania.

Warriors from the East pia watapanda jukwaani wakiwa ni washindi wa wimbo bora wa reggae, The African Stars wana wa kutwanga na kupepeta pia watapanda na tunzo yao ya wimbo bora kabisa uliowahi kutokea msimu huu wa Dansi, Ben Pol atapanda kama mwanamuziki bora wa R&B na Bi Khadija Kopa atawakilisha kama mtumbuizaji bora wa kike.Tamasha litaanza saa kumi jioni ambapo kila mtanzania mpenda burudani atatozwa kiingilio cha shilingi za kitanzania 4000 na pia atapatiwa bia moja bure mlangoni.

Kilimanjaro Premium Lager  inachukua fursa hii kuwakaribisha wadau wote wa burudani katika tamasha hili kubwa zuri, kuburudika na kutathmini kwa pamoja muelekeo wa sanaa yetu ya muziki.

DEREVA WA F 1 LEWIS HAMILTON ALIVYOZAMA MAPENZINI KWA MWANAMUZIKI NICOLE SCHERZINGER!!

COUNTING OF VOTES FOR EALA POLLS UNDERWAY!!

Casting of ballots for Uganda’s representatives to the regional Parliament has ended and counting of ballots is underway.

The Speaker of Parliament Rebecca Kadaga is presiding over the counting as a clerk reads out the names for tallying. 

Earlier, the Leader of Opposition in Parliament Nathan Nandala Mafabi exerted his authority and suspended UPC and DP from all Parliament opposition activities.

Nandala told the House that both parties defied the opposition position to boycott EALA elections until the Arusha Court ruling is enforced.  

MWANAMKE ANAEDAI KUZAA NA MBUNGE,ADAI MILIONI 1.2 KSH ZA MATUNZO YA MTOTO!!

Mbunge wa jimbo la Mwea Peter Gitau
Mwanamke raia wa Kenya anaedai kuwa ana mtoto wa miezi miwili aliyezaa na mbunge amedai shilingi za Kenya milioni 1.2 kutoka kwa mbunge huyo kwa ajili ya matunzo ya mtoto.

Hata hivyo  mbunge huyo wa jimbo la Mwea Bw. Peter Gitau amekana madai hayo akisema ameoa na ana familia yenye furaha.

Katika kesi hiyo iliyofunguliwa katika mahakama jijini Nairobi mwanamama huyo mwenye umri wa 21 anayefanya kazi katika kampuni binafsi amedai kuwa mbunge Gitau alimpa ujauzito na kisha kumtelekeza.

Ameendelea kudai kuwa mbunge huyo alimuahidi kumpatia kazi, gari na nyumba iwapo atamzalia mtoto.

TAYLOR AHUKUMIWA MIAKA 50 JELA!!

Rais wa zamani wa Liberia Charles Taylor leo amehukumiwa kifungo cha miaka 50 jela baada ya mwezi uliopita kutiwa hatiani kwa makosa ya uhalifu wa kivita na mahakama maalumu ya Umoja wa Mataifa huko The Hague hukumu iliyotolewa na Jaji Richard Lussick.

Waendesha mashtaka wa mahakama maalumu ya Sierra Leone waliitaka mahakama hiyo kumfunga mtuhumiwa huyo miaka 80 jela ambapo upande wa utetezi ulidai kuwa adhabu hiyo ni kubwa mno.

Taylor amesisitiza kuwa hana hatia na anatarajia kukata rufaa kupinga adhabu hiyo na mchakato wa rufaa unaweza kuchukua zaidi ya miezi sita.

Mahakama hiyo ilimtia hatiani Taylor kwa mashitaka 11 yanayohusiana na uhalifu wa kivita, ubakaji na mauaji.

May 28, 2012

WATU KADHAA WAJERUHIWA KATIKA MLIPUKO NCHINI KENYA!!

Majeruhi wakiingizwa kwenye gari la wagonjwa kukimbizwa hospitali
Watu kadhaa wamejeruhiwa nchini Kenya katika mlipuko ambao umetokea katika jumba la maonyesho karibu na jengo la Chuo Kikuu cha Mlima Kenya pembezoni mwa eneo lenye shughuli nyingi Moi.

Mlipuko huo ambao chanzo chake hakijajulikana mpaka sasa umetokea majira ya saa saba na robo mchana na kutingisha majengo yanayozunguka eneo hilo.

Jengo hilo linalojulikana kama  Assanands lilishika moto punde mlipuko huo ulivyotokea lakini vikosi vya zimamoto vimefanikiwa kuzima moto huo ambao umeunguza sehemu ya jengo.

Imeripotiwa kuwa bado kuna watu wamekwama ndani ya jengo ambalo ndani kuna maduka ya nguo.

May 24, 2012

NCHUNGA AJIUZULU UENYEKITI YANGA!!

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUHUSU KUJIUZULU NAFASI YA UENYEKITI WA KLABU YA YANGA.
Ndugu wana Habari, najua kwamba taarifa hii itawafedhehesha wajumbe na wanayanga wanaotuunga mkono,hasa ukizingatia maamuzi ya pamoja ya vikao vyetu vya kamati ya utendaji vilivyopita kwamba hakuna wa kujiuzulu kati yetu mpaka tujue hatma ya mkutano mkuu ambao tulipanga ufanyike tarehe 15 Julai 2012, ukiachia mbali shinikizo la kujiuzulu linalotolewa na baadhi ya wazee na wanaojiita vijana wa klab, kwa wajumbe wa kamati ya utendaji, na hasa mimi kama mwenyekiti.
Nawashukuru wajumbe kwamba tulifanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano mzuri, na hata pale tulipotofautiana tulifanya hivyo kwa hoja na kufikia maazimio ambayo wote tulikuwa tunawajibika nayo.
Tangu tumeingia madarakani tumeweza kushirikiana na kupata mataji matatu katika kipindi cha mwaka mmoja, yaani; Ngao ya Hisani 2010, Ubingwa wa ligi kuu ya Vodacom 2010/2011, na Ubingwa wa  Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup), 2011. Zaidi ni kwamba tuliuwa uteja kwa watani wetu wa jadi kila tulipokutana katika ligi ukiachia mbali mechi ya tarehe 6 Mei 2012, ambayo tulifungwa goli 5 bila, na kuleta mtafaruku mkubwa katika klab yetu.
Hali kadhalika tumeshirikiana  mpaka tumeweza kuboresha mkataba kati yetu na TBL kupitia Kilimanjaro Premium Lager, tumeingia mkataba na  kampuni ya NEDCO  kuendeleza mali zetu katika mtaa wa mafia na uwanja wetu wa KAUNDA baada ya kufikia hatua nzuri katika kupata hati miliki za maeneo yote mawili. Nafahamu kwamba kampuni hiyo iko katika hatua za mwisho za kumalizia michoro.
Hali kadhalika tuliingia mkataba wa kuzalisha na kuuza bidhaa zenye nembo yetu na hasa baada ya kufanya marekebisho yatokanayo na matakwa ya sheria kule BRELA na pia mkataba na kampuni ya NEXUS LTD, ambayo itakuwa inatutafutia wadhamini wa nje na ndani, kufanya promosheni zetu na kampeni kwa njia ya electronic kupitia mitandao mbalimbali na kukusanya data za wanachama na kusajili  wapya tukiwa na malengo ya kukusanya shilingi 300,000,000/= hadi 800,000,000/= kwa mwaka katika kipindi cha miaka mitatu. Haya yote tuliyafanya tukilenga kujitegemea kujazia mapengo yaliyokuwa yakitokana na kutegemea ufadhili wa mtu mmoja mmoja.
Kwa ridhaa yenu tumekua tukiendelea na mazungumzo na makampuni mbali mbali kwa ajili ya udhamini na kwa sababu maalum, nitazitaja katika hati ya makabidhiano kwa kiongozi ajaye.
Aidha, tumeshirikiana katika kufanya mambo mbali mbali ya kijamii, ikiwa ni pamoja na sikukuu ya kuadhimisha miaka 77 ya Yanga, sikukuu za pasaka, kuchangia jamii na waliokumbwa na maafa, na kongamano la vijana lililolenga kuwaamsha vijana kuitambua nafasi yao katika Yanga ikiwa ni pamoja na kupata azimio la kuanzisha SACCOSS ya Yanga, ambapo maombi yapo kwa msajili Manispaa ya Ilala.
Haya yote nayataja ikiwa ni kuwashukuru kwa ushirikiano na ikiwezekana muweze kuyakamilisha yaliyobaki ambayo mtaona yalikuwa mazuri.
Lakini pia tulipopata matatizo tulikuwa pamoja.  Nichelee kusema tu kwamba tulisimama pamoja baada ya kujiuzulu Makamu Mwenyekiti wetu Ndugu Davis Mosha na mjumbe wetu  ndugu Seif A. Seif, Ali Mayayi, na wengineo, kwani tulifungwa na katiba.Tulisimama pamoja pia katika suala la kujiuzulu ndugu Yusuf M. Manji, aliyekuwa mdhamini mteule na mfadhili mkuu ambaye sasa ameonyesha nia ya kurudi nanyi mkaridhia mkutane naye. Awali, tulitumia kila jitihada za kumrejesha lakini ikashindikana.
Hata hivyo doa limetupata baada ya kufungwa na watani wetu goli 5 bila, ambapo kuna wanachama wanaoelewa na wasioelewa kabisa.
Ninachokiona mimi ni usaliti wa hali ya juu uliombatana na matukio mbalimbali yaliyopita na yanayoendelea hadi kujaribu kupindua uongozi wa halali wa kidemokrasia. SIWATUHUMU WACHEZAJI MOJA KWA MOJA, isipokuwa  mfululizo wa matukio wiki tatu kabla ya mchezo ule na sasa, inaonyesha kwamba kulikuwa na usaliti mkubwa ambao sisi hatukuweza kuubaini mapema.
Sioni mantiki katika hoja kwamba wachezaji walikuwa wakidai mishahara, posho n.k.  Au ati mtendaji wetu alishikiliwa Arusha kwa deni la hoteli, ndiyo  tuvune bao 5!
Kwa wanaoijua Yanga, imewahi kuwa na madeni makubwa katika Hoteli mbali mbali, mawakala wa ndege n.k, na baadhi tumeyakuta na sisi tumekuja tukayalipa. Hii imewahi kutokea kabla na wakati akiwepo mfadhili, sembuse sisi tulioachwa baki, na bado wachezaji walicheza kwa morali.
Hata hivyo, utamaduni wa kutimuana baada ya matokeo mabaya ni dhambi ambayo itatula kama hatutaiacha, kwani wenye hila na uchu wa madaraka wataendelea kutumia mbinu hiyo ili kuuondoa uongozi wa kidemokrasia.
Baada ya mapinduzi kushindikana na TFF kuonya kuhusu mapinduzi hayo, wazee kupitia msemaji wao , Mzee Akilimali wamesikika katika kipindi cha Michezo  cha Redio moja maarufu hapa nchini wakidai kwamba ni bora Yanga ishushwe daraja au kufungiwa kuliko mimi kuendelea kuongoza!
Hii imenikumbusha HEKMA ZA MFALME SELEMANI akiamulia ugomvi wa wanawake wawili waliokuwa wakigombea mtoto naye akaamuru wamgawane nusu kwa nusu. Yule mwenye mtoto kweli alimuomba Mfalme amuachie mwenzie kuliko kumkata nusu.
Kwa hekma hiyo nimeamua kujiuzulu nafasi yangu katika Uenyekiti  wa Yanga kwani ni klab ninayoipenda hata kama sio kiongozi kwa mujibu wa ibara ya 28 ya katiba yetu.
Vile vile siko tayari kuona klab yangu ikisalitiwa au kuhujumiwa eti kwa sababu tu mimi ni kiongozi.
Natumaini kamati ya utendaji kwa pamoja na wale tuliowateua chini ya ibara ya 29(3) ya katiba ya Yanga pamoja na bodi ya wadhamini, itawaongoza wanachama mpaka kufikia mkutano mkuu kwa  mafanikio zaidi.
 Nitaendelea kuwa mwanachama mwadilifu na nitatoa mchango wangu wa hali na mali pale nitakapo hitajika na nikiwa  na uwezo wa kufanya hivyo.
YANGA DAIMA MBELE, NYUMA MWIKO.
Wasalaam,
LLOYD NCHUNGA BIHARAGU.
Nakala kwa:-
Mama Fatma Karume,Mdhamini
Francis Kifukwe, Mdhamini
Bwana Yusuf Manji – Kwa taarifa

LLOYD NCHUNGA BIHARAGU
C/O LLOYD ADVOCATES,
Morogoro/Bibi TIti  Mohamed Rd,7th Floor, J.K. Nyerere Pension towers
P.BOX 75111, Dar-Es- Salaam,Tanzania.

MNYIKA ASHINDA KESI!!

Mamia ya wafuasi wa CHADEMA wakiwa wamembemba mbunge John Mnyika ambaye ameshinda kesi katika hukumu iliyotolewa katika mahakama kuu kanda ya Dar es salaam.
Mbunge wa jimbo la ubungo nchini Tanzania John Mnyika, ameshinda shauri la kupinga ubunge wake liliofunguliwa katika mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam na aliyekuwa mgombe kupitia Chama Cha Mapinduzi Bi. Hawa Ng'umbi.

Jaji wa mahakama kuu, Upendo Msuya ametupilia mbali hoja zote tano zilizofikishwa mahakamani hapo na upande wa mashtaka kwa madai kuwa hoja hizo hazina msingi.

Akizungumza. Muda mfupi baada ya kutolewa kwa hukumu hiyo, mwenyekiti wa Chadema taifa, Freeman Mbowe amesema ushindi wa kesi hiyo ni ushindi kwa Watanzania wote huku akionyesha kusikitishwa na jinsi nchi inavyoingia hasara kwa kutumia kiasi kikubwa cha pesa kuendesha kesi zisizo na msingi.

TWIGA STARS YAKABIDHIWA BENDERA!!

Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanawake (Twiga Stars)  imekabidhiwa Bendera ya Taifa  tayari kuelekea nchini Ethiopia kucheza na timu ya nchi hiyo  katika mechi ya kwanza ya raundi ya pili ya michuano ya mchujo wa kucheza  Fainali za Nane za Kombe la Afrika kwa Wanawake (AWC) zitakazofanyika Novemba mwaka huu Equatorial Guinea.

Akikabidi bendera hiyo  Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Amos Makalla amesema anaamini wachezaji wamepata uzoefu wea kutosha katika michezo ya majaribio waliyocheza licha ya kufungwa..

Kwa upande wake kocha wa Twiga stars ameonyesha matumaini makubwa ya kushinda mchezo huo licha ya kuanzia ugenini.

Mechi hiyo itafanyika Mei 27 mwaka huu kwenye Uwanja wa Addis Ababa wakati ile ya marudiano itachezwa Juni 16 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Twiga Stars ikifanikiwa kuitoa Ethiopia itakuwa imepeta tiketi ya kwenda Equatorial Guinea.

RAIA WA MISRI WAENDELEA KUPIGA KURA!!

Zoezi la upigaji kura katika siku ya kwanza lilikwenda vizuri kwa utulivu katika maeneo mengi lakini waandamaji walirusha viatu na mawe katika ujumbe wa mgombea Ahmed Shafiq ambaye alikuwa waziri mkuu wa mwisho katika utawala wa Mubarak.

Baraza la kijeshi lililochukua madaraka mwezi Februari mwaka 2011 limeaahidi uchaguzi wa haki na utawala wa kiraia ambapo zoezi la upigaji kura lilianza jana kwa misururu mirefu iliyoonekana katika baadhi ya vituo vya kupigia kura.

Misururu mirefu imeonekana katika baadhi ya vituo vya kupigia kura na vyombo vya habari vimeripoti kuwa idadi kubwa ya watu wamejitokeza kuliko jana.

QATAR, DOHA, BAKU NA AZERBAIJAN NJE KATIKA KINYANG’ANYIRO CHA KUANDAA OLIMPIKI 2020!!

Miji ya Tokyo, Madrid na Istanbul ndiyo iliyobakia katika kinyang’anyiro cha kuwania nafasi ya kuandaa mashindano ya Olimpiki ya mwaka wa 2020.

Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki – IOC iliyokutana mjini Quebec nchini Canada imepunguza orodha ya miji iliyokuwa ikiwania nafasi hiyo, ambapo mji mkuu wa Qatar -Doha, Baku na Azerbaijan imeondolewa katika orodha hiyo.

Kamati ya Olimpiki itafanya maamuzi ya mwisho mnamo Septemba 7 mwaka 2013, kuhusu mji upi upewe fursa ya kuandaa mashindano ya Olimpiki ya majira ya joto yatakayofanyika mwaka 2020. 

Mashindano ya mwaka huu yatafanyika katika jiji London nchini Uingereza.

May 22, 2012

AGRA TO HELP IMPLEMENT NEW G8 GLOBAL PARTNERSHIP INITIATIVE ON FOOD SECURITY!!

The Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA) was given a key role in the G8’s next phase.

The Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA) (http://www.agra-alliance.org) was given a key role in the G8’s next phase of a shared commitment to achieve global food security. The Scaling Seeds and Other Technologies Partnership, part of the new initiative focused on increasing agricultural food production in Africa, will be housed at AGRA and will focus on strengthening Africa’s seed sector.

“African food security will only be met by increased agricultural production,” said Strive Masiyiwa, AGRA’s acting chair addressing the G8 leaders and four African heads of state at the G8 Summit. ” The approach being put forward by the G8 is modeled on some of AGRA’s on-going work on behalf of Africa’s smallholder farmers and we are pleased to play a major role in this global initiative.”

The Scaling Seeds and Other Technologies Partnership will strengthen the seed sector and promote the commercialization, distribution and adoption of key technologies improved seed varieties, and other technologies to meet concrete targets in partner countries.  AGRA has been working since its creation five years ago through many partners to create breadbaskets in Africa through support to millions of smallholder farmers.

“AGRA is working with its main partners to create breadbaskets in Africa through support to smallholder farmers,” said Jane Karuku, AGRA President.  “We are now seeing smallholder farmers prospering due to bigger crop yields and entire communities benefiting from the growth of small agribusinesses.”

Particularly impressive are results in significantly boosting staple crop production. Through the support of AGRA and its partners, an additional 40,000 metric tons per annum of hybrid seed, representing one-third  of the commercially produced seed in Africa, is now reaching smallholder farmers. These seeds have been produced by 60 small, African-owned seed companies launched with capital and strengthened by AGRA – a 100 percent increase in the number of such companies. In terms of food production, this means an additional four million metric tons of staple crops per annum.  AGRA’s experts believe that the tipping point to food security with respect to improved seeds is 500,000 metric tons per annum of high yielding, improved crop varieties.

AGRA has invested in training African scientists who will develop research capacity, and strengthen the capacity of seed companies both technically and in terms of management capability. It has established MSc and PhD programs at 13 key African universities – more than 400 post- graduate students have been enrolled, a hundred of whom have graduated. This represents a quarter of the scientists known to be working in this field today. AGRA’s  experts believe that 1,000 new scientists in this field are required to sustain the Green Revolution. To date, these and other AGRA-supported scientist have produced 342 new crop varieties – a 100 percent increase in available improved varieties.

AGRA has developed almost 15,000 agro-dealer businesses, which are an integral part of the value chain in sustaining a private sector-led, market oriented agriculture sector. 

In partnership with African governments and their central banks, as well as domestic and international banks, AGRA has pioneered innovative, risk sharing, finance schemes that have already allowed millions of smallholder farmers in 6 countries to access nearly 1 billion dollars in credit from their own banking systems for the first time.

ATIWA MBARONI KWA UTAPELI KUJIFANYA BWANA AFYA!!

Mtuhumiwa Bw. Swalehe Mshana akiwa chini ya ulinzi mkali
Ofisi ya Afisa mtendaji wa kata ya Kinondoni jijini Dar es salaam imemtia mbaroni mmoja wa watu wanaodaiwa kuwa ni matapeli kwa kusema wao ni mabwana afya na hatimaye kuchukua fedha kwa njia za udanganyifu kutoka kwa wananchi.

Mtuhumiwa huyo Bw. Swalehe Mshana mkazi wa jiji la Dar es salaam alikamatwa na kufungwa pingu na kufikishwa katika ofisi za kata ya Kinondoni ambapo amekuwa akijifanya bwana afya na kuwakagua watu na kisha kuwachukulia fedha.

GLOBAL WARNING ON YOUTH JOBLESS!!

Almost 13% of young people worldwide are out of work, and their situation is unlikely to improve for four years, a report by the International Labour Organization (ILO) says.


Many skilled young people are being forced into part-time and unskilled work, the report says.


It warns of a "crisis" with more than six million people so disillusioned they have given up looking for work.


The ILO wants governments to make job creation a priority.


It wants more training schemes, and also tax breaks for employers.

RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE AMUAPISHA PROFESA MARK MWANDOSYA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM LEO!!

Waziri wa nchi katika ofisi ya Rais asiye na Wizara maalum Profesa Mark Mwandosya akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue.Na watatu kulia ni Karani wa Baraza la Mawaziri Bwana Gerson Mdemu.

BOMOA BOMOA YAWAKUMBA WASUSI AMANA!!

Askari wa jiji wakiwa kazini kubomo vibanda vya wasusu maeneo ya Ilala Amana leo asubuhi
Wajasiriamali wanaojishughulisha na biashara ya ususi pembezoni mwa ukuta wa amana Ilala jijini Dar esa salaam nchini Tanzania mapema leo asubuhi wamekumbwa na dhahama ya bomoa bomoa ya vibanda vya kufanyia shughuli zao kwa kile kilichoelezwa kuwa chanzo ni migogoro ya wao kwa wao.

Zoezi hilo lililofanyika mapema leo limeelezwa kuwa chanzo chake ni kutoelewana wao kwa wao ambapo Manispaa ya Ilala imeamua kuchukua uamuzi wa kutatua mgogoro huo kwa kubomoa vibanda kitendo kilichoelezwa na wasusi ni kuepusha athari nyingine kubwa ambayo ingeweza kutokea kutokana na ubabe wa wachache kuwanyanyasa wasio kuwa na uwezo.

RAIS WA MUDA MALI ASHAMBULIWA NA WAANDAMANAJI!!

Rais wa muda Mali Bw. Dioncounda Traore
Wakuu wa serikali nchini Mali wamesema kuwa Rais wa muda wa nchi hiyo Bw. Dioncounda Traore amepelekwa hospitali akiwa na jeraha kichwani baada ya kushambuliwa na mamia ya waandamanaji.

Rais huyo anadaiwa kuwa alikuwa amezirai wakati anafikishwa hospitalini hapo lakini baadae aliruhusiwa.

Jeshi la nchi hiyo limesema kuwa limewauwa kwa kuwapiga risasi watu watatu wakati wa maandamano hayo makubwa yaliyosababishwa na kupinga mkataba ulioafikiwa kwa Bw. Traoure kuendelea kutawala kwa hadi mwaka mmoja badala ya siku 40 pekee zilizokubaliwa miezi miwili iliyopita.

DALADALA YAZAMA MTARONI JIJINI DAR!!

Picha juu na chini wananchi waliofika eneo la tukio wakijaribu kulitoa gari hilo wakisaidina Break down
Daladala moja linalofanya safari zake kati ya Ubungo-Msasani jijini Dar es salaam lenye namba za usajili T774 BKE lililokuwa likijaribu kulipita jingine limepinduka na kuingia mtaroni katika eneo la Makutano ya barabara ya ubalozi wa Marekani na Old Bagamoyo.

Ajali hiyo imetokana na kile kilichodaiwa kitendo cha maderez=va wanaoendesha daladala kushindana kuwahi abiria kutoka kituo kimoja hadi kingine na kuendelea kusababisha ajali mbalimbali kutokana na haraka na kupita barabara zisizo sahihi.

Abiria waliokuwa ndani ya gari hilo wameumia na kupata majeraha madogo madogo ambapo mashuhuda wamesema uzembe wa dereza wa gari hilo umesababisha ajali hiyo.

May 21, 2012

MWASISI WA FACEBOOK AFUNGA NDOA NA MPENZI WAKE WA SIKU NYINGI!!

Mwasisi wa mtandao maarufu wa kijamii Facebook Mark Zuckerberg amefunga ndoa mwishoni mwa wiki iliyopita na mpenzi wake wa siku nyingi Priscilla Chan, Harusi hii imeripotiwa kuwa ya kipekee na mvuto mkubwa katika mitandao mbalimbali ya burudani ya kimataifa.

Wawili hawa walikutana huko Harvard na wamekuwa pamoja kwa miaka 9 sasa, kabla ya kuamua kufunga ndoa na kufanya sherehe ndogo nyumbani kwa Zuckerberg huko Palo Alto, Calif.

Mke wa Zuckerberg alihitimu masomo yake ya udaktari katika chuo cha California muda mfupi kabla ya harusi yake na majirani waliyoizugumzia sherehe ya harusi hiyo wamesema kuwa walisikia miziki mbalimbali ya wasanii kama Flo Rida, Bon Jovi na Janet Jackson ila miziki iliyopigwa zaidi ilikuwa ni ile ya marehemu Michael Jackson.

MAZIKO YA MEGRAHI YAFANYIKA!!

Megrahi alihamishwa kutoka gereza la Scotland mwaka 2009 akiwa anaugua saratani
Maziko ya Mtu aliyeshtakiwa kwa kuilipua ndege kwa mabomu Lockerbie mwaka 1988 Abdelbaset al-Megrahi ambaye amefariki dunia nyumbani kwake Tripoli jana yamefanyika nyumbani kwao huko Tripoli.

Megrahi ni mtu pekee aliyeshtakiwa kwa kulipua ndege hiyo iliyosababisha vifo vya takribani watu 270 ambapo alishtakiwa na mahakama maalum huko Uholanza mwaka 2001.

Megrahi alihamishwa kutoka gereza la Scotland mwaka 2009 akiwa anaugua saratani ambapo waziri mkuu wa Uingereza Bw. David Cameroon amesema ni siku ya kukumbuka wahanga 270 waliokufa katika tukio hilo kubwa la kigaidi.

WILL SMITH AMNASA KIBAO MWANDISHI WA HABARI!!

Mwanamuziki na mcheza filamu kutoka nchini Marekani Will Smith ameripotiwa kwa tukio la kumnasa kibao mwandishi wa habari raia wa Ukraine, Vatalii Sediuk, baada ya jaribio lake la kumbusu mdomoni nyota huyo kushindikana.

Smith kwa sasa yupo katika kampeni na vyombo vya habari kutangaza toleo lake la tatu la filamu ya Men In Black ambayo inatarajiwa kutoka rasmi mei 25.

Katika Red Carpet party iliyofanyika huko Moscow, Seiduk wakati akikumbatiana na Will Smith alijaribu kumbusu Smith mdomoni, kitendo ambacho kilimuudhi na kumshangaza sana hadi kushindwa kujizuia kurusha kofi.

WATU WATATU WAMEKUFA JUU YA MLIMA EVEREST!!

Maafisa huko Nepali wamesema kuwa Takribani watu watatu wamefariki dunia wakati wakirejea kutoka kilele cha mlima Everest,Nepali.

Kitengo cha wapanda milima huko Gyanendra Shresth kimesema kuwa watu hao watatu wanaaminika kuwa ni raia kutoka Korea kusini,Mjerumani mmoja na mwanamke kutoka nchini Canada ambapo hali zao zilikuwa kawaida siku za Ijumaa na Jumamosi asubuhi lakini upepo mkali ulipiga mlima humo baadae.

Pia kitengo hicho kimeongeza kuwa wapanda mlima wengine wawili kwa sasa wamepotea.

May 10, 2012

MWENGE WA OLIMPIKI WAWASHWA UGIRIKI!!

Moto wa mwenge utakaotumiwa kuwasha mwenge wa mashindano ya Olimpiki mjini London uliwashwa mahali yalipozaliwa mashindano ya kale ya Olimpiki siku ya Alhamisi.

Muigizaji mwanamke, aliyevalia kama mtawa mwanamke wa enzi za miungu wa Kigiriki alitumia kioo kupokea mwanga wa jua na kuasha mwenye.

Kukiwa na jua la kutosha angani, hapakua na sababu ya kutegemea moto kutoka kwingine wakati wa kufanya majaribio ya mwisho kuasha mwenge wa Olimpiki siku moja kabla.

Baada ya sherehe za kufana, mtawa huyo atakabidhi mwenge kwa mtu wa kwanza kutembeza mwenge huo, mwanariadha muogeleaji kutoka Ugiriki aliyeshinda medali ya fedha kwenye mashindano yya Olimpiki Spyros Gianniotis.

OBAMA AUNGA MKONO NDOA ZA JINSIA MOJA!!

Rais wa Marekani Bw. Barack Obama
Rais wa Marekani Bw. Barack Obama amemaliza mwezi mmoja wa majadiliano juu ya suala la ndoa za jinsia moja na kusema watu wa jinsia moja wawe na haki ya kuoana.

Rais Obama anakuwa rais wa kwanza wa Marekani kukubaliana na
suala hilo la ndoa ya jinsia moja.

Mpinzani wake katika uchaguzi wa rais wa mwaka huu, Mitt Romney, wa chama cha Republican amesema bado anabakia kupinga ndoa za watu wa jinsia moja.

Siku za karibuni Makamu wa rais Joe Biden na mmoja wa mawaziri Arne Duncan walielezea kuunga mkono vyama vya watu wanaojihusisha na mapenzi ya jinsia moja.

Katika shambulio la bomu lilitokea mwishoni mwa mwezi Aprili ambapo watu 10 waliuwawa karibu na msikiti.

MABOMU YAPIGWA SYRIA!!

Milipuko miwili imepiga katika mji mkuu wa Syria  Damascus huku kituo cha Televisheni cha nchi hiyo kikisema kuwa mamia ya watu wameuwawa na wengine kujeruhiwa katika shambulio hilo la kigaidi.

Katika picha za video za mlipuko zimeonyesha uharibifu mkubwa katika kitongoji cha  al-Qazzaz kusini mwa mji wa Damascus.

Mji huo umekuwa ukilengwa na mashambulio kadhaa ya mabomu katika miezi ya hivi karibuni kufuatia mgogoro wa kupinga serikali yua nchi hiyo.

May 9, 2012

RAIS KIKWETE AWASILI ADDIS ABABA KWA KONGAMANO LA UCHUMI LA KIMATAIFA KWA AFRICA!!


 "Karibu Mheshimiwa...." Anaonekana kusema Mkurugenzi wa World Economic
Forum kwa Afrika Bi Elsie Kanza wakati wa kumpokea Rais Jakaya Kikwete
alipowasili hoteli ya Sheraton jijini Addis Ababa usiku wa kuamkia leo
April 9, 2012 tayari kuhudhuria Kongamano la Uchumi la Kimataifa kwa Afrika
linaloshirikisha zaidi ya viongozi 700 wa nchi, biashara na uchumi kutoka
sehemu mbalimbali duniani.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa USAID Dkt Rajiv
Shah katika hoteli ya Sheraton jijini Addis Ababa leo April 9, 2012 ambako
kwa pamoja wanahudhuria Kongamano la Uchumi la Kimataifa kwa Afrika
linaloshirikisha zaidi ya viongozi 700 wa nchi, biashara na uchumi kutoka
sehemu mbalimbali duniani
Rais Jakaya Kikwete katika maungumzo na Mkurugenzi Mkuu wa USAID Dkt
Rajiv Shah katika hoteli ya Sheraton jijini Addis Ababa leo April 9, 2012
ambako kwa pamoja wanahudhuria Kongamano la Uchumi la Kimataifa kwa Afrika
linaloshirikisha zaidi ya viongozi 700 wa nchi, biashara na uchumi kutoka
sehemu mbalimbali duniani.(PICHA NA IKULU)

TANZANIA YATOA MSIMAMO WAKE JUU YA MGOGORO WA MOROCCO NA SAHARA MAGHARIBI!!

Waziri wa mabo ya nje wa Tanzania Mhe. Bernard Membe akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo.
Nchi za Afrika zimetakiwa kuwa makini dhidi ya tishio jipya ya mgawanyo wa bara la Afrika kutokana na uchu wa mataifa ya kigeni, dhidi ya rasilimali za bara hilo kama ilivyofanywa na wakoloni huko jijini Berlin Ujerumani mwaka 1884.

Waziri wa mambo ya nje wa Tanzania,Bernard Membe amesema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati akielezea msimamo wa Tanzania kuhusu harakati za Sahara Magharibi za kutaka kutambuliwa kama taifa huru nje ya utawala wa Morocco.

Kwa mujibu wa waziri Membe, nchi za Ulaya, Asia na Amerika zimekuwa zikifanya harakati ya kuchukua rasilimali na kujenga mtandao wa masoko ya bidhaa zao barani Afrika, kupitia mikataba ya isiyo na maslahi kwa Waafrika wenyewe.

Amewataka viongozi wa Afrika kutumia mkutano wa kimataifa wa uchumu unaoendelea jijini Addis Abbaba Ethiopia, kufikia maazimio yatakayohakikisha ulinzi wa rasilimali za Afrika dhidi ya tishio hilo.

May 7, 2012

WAZIRI MKUU ODINGA AIFUKUZA BODI YA NHIF KENYA AKIKINZANA NA KAIMU MKUU WA UTUMISHI WA UMMA ALIYEIREJESHA KAZINI!!

Waziri mkuu wa Kenya Raila Odinga leo ameifukuza kazi bodi ya mfuko wa taifa wa bima ya afya na mtendaji wake mkuu kufuatia uamuzi wa waziri wa huduma za jamii Anyang' Nyong'o.

Waziri mkuu Odinga amemteua kaimu katibu mkuu wa wizara hiyo A. Adan kuwa kaimu mkurugenzi mkuu ambapo pia ameiteua bodi ya uangalizi inayoundwa na makatibu wakuu na wawakilishi kutoka vyama vya Cotu na Knut.

Tangazo la waziri mkuu Odinga linakinzana na tangazo la kaimu mkuu wa utumishi wa umma Francis Kimemia la kuifukuza bodi hiyo na mkurugenzi wake mkuu.        

RAIS KIKWETE AWAAPISHA MAWAZIRI NA NAIBU MAWAZIRI ALIOWATEUA IKULU JIJINI DAR ES SALAAM!!

Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dk. Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika viwanja vya Ikulu asubuhi hii ili kuanza kazi ya kuapisha mawaziri wapya aliowateua hivi karibuni katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam.
Dk. Harrison Mwakyembe akila kiapo kuwa Waziri wa Uchukuzi mbele ya Rais Jakaya Kikwete kwenye viwanja vya Ikulu asubuhi hii.
Mhe Hawa Ghasia akila kiapo mbele ya rais Jakaya Kikwete
Dk. Hussein Mwinyi akila kiapo kuwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii mbele ya rais Jakaya Kikwete

26 DEAD,100 MISSING IN ARGHANISTAN FLOOD!!

Flash flooding in northern Afghanistan killed at least 26 people in northern Afghanistan and rescue workers fear the toll may rise, officials said Monday.


Eight hours of relentless rainfall that began Sunday led to the flooding in several districts of Sar-e-Pol province, said Faizullah Sadat, provincial director of Afghanistan Disaster Management Authority (ANDMA).


More than 100 people are missing, most of them members of a wedding party that was deluged, he said.
SOURCE:CNN

CAG AWAONYA MAWAZIRI WAPYA!!

CAG Ludovick Utouh
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh amewaonya mawaziri wapya na watendaji serikalini kwamba ripoti zake hivi sasa zina nguvu za kusimamia uwajibikaji hivyo, wanapaswa kusimamia vyema wizara zao kuzuia ubadhirifu wa fedha za umma.

Kauli hiyo ya Utouh ni ya kwanza tangu ripoti yake ya mwaka huu kuwang’oa mawaziri sita kati ya wanane ambao wizara zao zilionekana kugubikwa na ufisadi wa fedha za umma.

Akizungumza jana, Utouh alisema mawaziri wanapaswa kufahamu kwamba kuanzia sasa hadi mwaka 2015, zitatoka ripoti nyingine tatu, hivyo ni vyema wakachukua tahadhari wakiwa ndiyo wasimamizi wakuu wa shughuli za wizara.

Alisema kilichotokea bungeni na hadi mawaziri kuwajibishwa, kimethibitisha kuwa sasa kutakuwa na uwajibikaji mkubwa utakaosababishwa na ripoti zake kama watendaji wasipofuata taratibu za Serikali.

PUTIN AAPISHWA KUWA RAIS WA URUSI!!

Rais wa Urussi aliyechaguliwa hivi karibuni Vladimir Putin ameapishwa leo katika sherehe zilizofanyika katika mji mkuu wa nchi hiyo  Moscow.

Putin anarejea katika urais baada ya miaka minne ambayo alikuwa waziri mkuu wa nchi hiyo chini ya rais Dmitry Medvedev,ambaye inasemekana ni mshirika wa karibu wa Putin.

Putin ameshinda urais kwa muhula wa tatu katika uchaguzi ambao uligubikwa na utata uchaguzi uliofanyika mwezi8 March mwaka huu,jana maelfu ya waandamanaji walipambana na polisi wakipinga kuapishwa kwa Putin.

MESSI AVUNJA REKODI YA DUNIA!!

Mshambuliaji Lionel Messi alifunga mabao manne na kutegeneza rekodi mpya yakufunga mabao 72 msimu huu na kumwanga kocha wa Barcelona, Pep Guardiola kwa ushindi 4-0 dhidi ya Espanyol ukiwa ni mchezo wao wa mwisho kucheza Camp Nou msimu huu.

Messi alifunga mabao hayo na kutoa zawadi kwa kocha wake aliyemsaidia Margentina huyo kuwa mchezaji bora wa dunia na Barcelona kuwa timu bora zaidi duniani.

Baada ya kufunga bao lake la 50 katika La Liga msimu huu, Messi alikimbia na kumrukia Guardiola, ambaye anaondoka baada ya kutwaa mataji 13 katika misimu nne.

Mchezaji mwingine aliyefunga mabao 70 katika msimu moja wa ligi daraja la kwanza ni Archie Stark akiwa na timu ya Bethlehem Steel iliyokuwa ikishiriki Amerikani Soka Ligi (MSL) ulikuwa ni msimu wa 1924-25.

WAWAKILISHI WA TANZANIA BIG BROTHER STAR GAME!!

Hilda
Biography:

Hilda hails from Morogoro and is a saleswoman. She has a son and enjoys the novels of Sydney Sheldon and the book Memoirs of a Geisha. Hilda was inspired to enter Big Brother StarGame by Biggie himself! “He seems to be a big challenge in the House and so I thought it would be fun to join him this time around and give him a special challenge. I can’t wait…” she says. She’s excited by the partnering format of this year’s show as it will be filled with fun and entertainment – plus her partner Julio is her best friend. “He is charming, sweet and a very good listener, of course,” she says.


She says she will do whatever it takes to win the grand prize – including lying her way out of a tricky situation or “being the sweetest thing ever”. She knows that Africa will be talking about her as soon as they see her on screen – which makes her excited. She says if she wins, she will donate money to a charity she supports back home as a peer health educator to help them build a nice house

Julio
Biography    


Julio is from Dar es Salaam and works as the Head of VAS, Electronic Channels and Products at a company in the telecommunications industry. With a BComm in Finance and an MBA under his belt, he looks set to be a wily player on Big Brother StarGame! He entered to be on the show because his best friend – Hilda – was the perfect example of the best candidate. Coupled with that, he saw himself as the most complete character because of how he lives his life as a hedonist.


He says of his partner Hilda that she is “real and straightforward” and that he’s always comfortable when she’s around. He says that men adore her while women are always on his case. “She’s smart, very interesting – especially with how much she knows, Africa will love her to death,” he says. He’s a fan of the show and cites Kevin as his favourite Housemate, though he says “at the end of the day, he has nothing on what I’ll bring to the House”.


Julio describes himself as fun, crazy, smart, cunning and entertaining.