Chama cha wamiliki wa mabasi nchini Tanzania TABOA leo kinakutana na wadau mbalimbali wa usafiri wakiwemo viongozi wa Halmashauri ya jiji la Dar es salaam, Sumatra, Jeshi la polisi na wadau wengine ili kuweka mikakati ya kudumu ya kupambana na tatizo la wapiga debe katika kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani Ubungo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mjumbe wa kamati ya utendaji ya TABOA Rajab Kassim amesema kwa sasa kero hiyo imepungua kwa zaidi ya asilimia 80 kufuatia kampeni ya kuwaondoa wapiga debe katika eneo hilo.
Amesema kampeni hiyo ilifanywa na Taboa pamoja na halmashauri ya jiji kwa kipindi cha wiki mbili hadi sasa inayowashirikisha pia polisi na askari wa ulinzi shirikishi waliopo chini ya chama hicho ambayo kwa kiasi kikubwa imefanikiwa kuwaondoa wapiga debe hao.
No comments:
Post a Comment