HOME

May 16, 2013

POULSEN AWATEMA KIKOSINI CHOLO NA NDITI!!


Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania,Taifa Stars, Kim Paulsen ametangaza kikosi cha wachezaji 24 watakaoingia kambini Mei 20 mwaka huu kujiandaa na mechi dhidi ya timu ya taifa Morocco mchezo utakaopigwa June 6 mwaka huu, mjini Marakesh nchini Morocco.

Akitangaza kikosi hicho leo jijini Dar es salaam, Paulsen  amewatema wachezaji Issa,Cholo na Nditi huku akiwaita wachezaji wanne ambao hawakuwepo katika kikosi cha awali

Poulsen amesema kabla ya Taifa Stars kucheza na Morocco itacheza mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Sudan mchezo utakaopigwa june 2 mwaka huu jijini Addis Ababa nchini Ethiopia.

No comments:

Post a Comment