HOME

May 21, 2013

PROFESA JAY AJIUNGA RASMI CHADEMA!!

Msanii nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania Joseph Haule maarufu kama Professor Jay amejiingiza rasmi katika siasa kwa kujiunga na chama cha siasa cha upinzani cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Professor Jay amefikia uamuzi huo leo Jijini Dodoma, na kukabidhiwa kadi ya CHADEMA na Mbunge wa Mbeya Mjini kwa tiketi ya CHADEMA Mhe. Joseph Mbilinyi ambaye mbali na siasa nae pia ni msanii wa muziki wa rap anayejulikana katika fani kwa jina la Sugu.
Profesa Jay bado yupo mjini Dodoma katika harakati zake hizo za kujiunga na siasa ambapo ameambatana na wasanii mbalimbali akiwemo Lady Jay Dee, Mapacha , Rama Dee na King Kiboya kwenye picha hapo chini.
Jay amekuwa gumzo kwa siku ya leo haswa kutokana na kutangaza uamuzi huo na ku tweet picha nyingi kupitia akaunti yake ya Twitter ambazo zimetumika na mitandao mbalimbali (Ukiwemo huu) zikimwonyesha akifurahia kila hatua aliyokuwa akipiga katika harakati zake kiaiasa.
Kila la Kheri Profesa tunasuburi mwendelezo wa harakati zako pale utakapotutangazia kwamba utagombea Ubunge katika Jimbo lako na kuongeza idadi ya wasanii wanaharakati wenye uzalendo wa kweli na nchi yao katika kutetea maslahi ya wasanii na wananchi kwa ujumla.


No comments:

Post a Comment