HOME

May 23, 2013

SERIKALI YATOA TAARIFA BUNGENI KUHUSU GESI MTWARA!!

Waziri wa mambo ya ndani nchini Tanzania Mhe. Emanuel Nchimbi ametoa taarifa fupi leo bungeni mjini Dodoma kuhusiana na vurugu zilizoibuka jana mkoani Mtwara nchini Tanzania kuhusu sakata la gesi iliyogunduliwa katika mkoa huo.

Kwa niaba ya waziri mkuu, Mhe. Nchimbi amewasilisha taarifa hiyo akielezea kiini cha vurugu, madhara pamoja na hatua ambazo serikali imeshachukua mpaka sasa ikiwemo kuwakamata baadhi wa waliohusika kwa namna moja au nyingine katika kuchochea vurugu.
Waziri Nchimbi amesema kuna kikundi cha watu ambao walihamasiha watu kuandamana siku ya jana na kusitisha huduma zote na kijamii ikiwemo maduka na migahawa ambapo hata hivyo makundi ya vijana walikusanyika kukisikiliza hotuba ya bajeti ya wizara ya nishati na madini iliyokuwa ikiwasilishwa jana na kuanza kuchoma matairi barabani ikiwa ni pamoja na kupanga mawe makubwa.


Kati ya madhara yaliyotokea kufuatia vurugu hizo ni pamoja na kuchoma Ofisi ya mbunge wa chama cha mapinduzi ambayo imeharibiwa vibaya, mahakama ya mwanzo imechomwa na kuteketea kabisa, Nyumba ya askari polisi imechomwa, nyumba ya mwandishi wa habari wa TBC ilichomwa ambapo mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Karim Shaibu amefariki dunia na askari wawili kujeruhiwa.

''Mpaka sasa Watuhumiwa 91 wamekatwa kwa kuhusika na mikusanyiko isiyo na kibali ambapo Wakati huo askari wanne walipoteza maisha wengine kujeruhiwa wakati wakiwa njiani kwenda kulinda maisha ya watanzania  mkoani Mtwara na kwakuwa waliumia wakiwa kazini damu yao haitamwagika bure''. Nchimbi

Nchimbi amesema suala hilo limekwishazungumziwa sana ikiwemo faida zake na usafirishwaji wake kwa uchumi wa nchi. Wasaliti wanatumia vibaya uelewa wetu mdogo kuhusiana na gesi hivyo tusikubali kuyumbushwa.


Kufuatia suala hilo, Spika wa bunge la Tanzania Mhe. Anna Makinda amelazimika kuahirisha shughuli za bunge hadi kesho saa tatu asubuhi na kuitaka kamati ya uongozi kukutana kujadili kwa kirefu zaidi suala hilo kuhusiana na vurugu zilizotokea jana mkoani Mtwara.

Picha kwa hisani ya

No comments:

Post a Comment