HOME

May 24, 2013

MJUKUU WA MALCOM-X AUAWA, AZIKWA SIKU MBILI BAADA YA BIRTHDAY YA BABU YAKE!

Siku ya tarehe 9 May mwaka huu, dunia ilimpoteza mwanaharakati mwingine Malcom Shabazz ambaye ni mjukuu wa aliyekuwa mwanaharakati wa kimarekani wa haki za binadamu Malcom X.


Malcom Shabazz aliuawa baada ya kutokea ugomvi kwenye bar ya Palace huko Mexico City, kwa kile kilichodaiwa kuwa alikuwa na deni la kiasi cha $1,200. Wafanyakazi wawili wa bar hiyo David Hernandez Cruz na Manuel Alejandro Perez de Jesus, wanashikiliwa na polisi kwa mauaji hayo. 

Shabazz alizikwa pembeni mwa babu na bibi yake kwenye makaburi ya Ferncliff Hartsdale New York, tarehe 21 May, ambayo ni siku mbili baada ya birthday ya babu yake Malcom X, ambaye angetimiza miaka 88 kama angekuwa hai leo.

MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI, AMEN!

No comments:

Post a Comment