Mrisho Ngassa akiibusu jezi ya Yanga baada ya kutambulishwa rasmi kurejea katika klabu hiyo kwa mkataba wa miaka miwili asubuhi ya leo katika Makao ya klabu hiyo Makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, jijini Dar es Salaam.
Klabu ya soka ya Yanga imetangaza kumsajili mchezaji Mrisho Ngasa kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu pamoja na michuano ya kimataifa.
Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, katibu mkuu wa Yanga Lawrence Mwalusako amesema kuwa klabu hiyo imemsajili mchezaji huyo kwa mkataba wa miaka miwili kwa ada ya uhamisho ambayo haijawekwa wazi.
Hivi katibuni kumekuwa na tetesi za muda mrefu ambazo zimekuwa zikimhusisha mchezji huyo kurejea Yanga ambapo hapo jana mchezaji huyo aliichezea Simba katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu Tanzania bara msimu huu.
(Picha kwa hisani ya Afisa Habari wa Yanga Baraka Kizuguto)
No comments:
Post a Comment