HOME

May 3, 2013

TANZANIA KUWA MWENYEJI WA MKUTANO WA SMART PARTNERSHIP!!

Tanzania inatarajia kuwa mwenyeji wa mkutano wa kimataifa wa Ushirikiano Wenya Manufaa kwa Wote unaolenga kutafuta mbinu mpya za kukuza uchumi na maendeleo ya kijamii maarufu kama Smart Partnership.







Mkuu wa sekretarieti inayoratibu mkutano huo Bi. Victoria Mwakasege (Katikati) kutoka wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa amesema jumla ya wageni 600 kutoka sehemu mbali mbali duniani, kati yao wakiwemo wakuu wa nchi watahudhuria 
mkutano huo utakaoanza Juni 28 na kumalizika Julai Mosi.
Waandishi wa habari wakipata taarifa kuhusu mkutano huo wa Smart Patnership katika Ukumbi wa kurugenzi ya habari na mawasiliano Ikulu, Jijini Dar es salaam.
Meneja wa Sekretariti inayoratibu mkutano huo Bi. Rosemary Jairo akifafanua kwanini Tanzania imeamua kuwa mwenyeji wa mkutano huo na faida itakazopata kutokana na mkutano huo ambapo amewataka waandishi wa habari kuwa wazalendo katika kuripoti habari chanya zinazohusu mambo mbalimbali ya maendeleo.
Bi. Mwakasege amezitaja faida nyingi zitakazopatikana kutokana na mkutano huo kuwa ni pamoja na manufaa ya kiteknolojia hususani namna ya kutekeleza majukumu ya kuihudumia jamii





 

No comments:

Post a Comment