HOME

May 22, 2013

RAIS JOYCE BANDA AKERWA NA TABIA YA WANAWAKE KUTOPENDANA!!




























Rais wa Malawi Bi. Joyce Banda amelalamikia tabia ya
wanawake kutoungana mkono tatizo ambalo amesema lipo dunia nzima.


Akiongea kwenye mahojiano ya kipindi cha televisheni ya Al Jazeera, Bi. Banda amesema kumekuwa na hali ya wanawake kutotaka kunyanyuana wao kwa wao.

Banda ambaye ni rais wa pili mwanamke barani Afrika baada ya Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia, aliingia madarakani Aprili mwaka jana kufuatia kifo cha Rais Bingu wa Mutharika.

Joyce Banda amesema kuwa tangu aingie madarakani ameshangazwa namna wanaume wanavyomuunga mkono katika utendaji wa serikali yake.

No comments:

Post a Comment