HOME

May 16, 2013

MATUMIZI YA SIMU BARABARANI YACHANGIA AJALI NYINGI!!

Matumizi ya simu wakati wa kuendesha vyombo vya usafiri wa nchi kavu na matumizi ya simu wakati wa kutumia barabara yameelezwa kuchangia kwa kiasi kikubwa ongezeko la ajali na kupoteza maisha ya Watanzania walio wengi.


Hayo yamelezwa leo jijini DSM na Mkuu wa Jeshi la polisi Kikosi cha Usalama barabarani nchini Tanzania Kamanda Mohamed Mpinga wakati Tanzania ikiungana na nchi nyingine Duniani kuadhimisha wiki ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).

Aidha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano nchini Tanzania TCRA Prof. John Nkoma ameeleza kwamba kwa kuwa maadhimisho ya wiki ya TEHAMA mwaka huu yanabeba kauli mbiu ya “Tehama katika kuboresha ya  usalama barabarani” wameamua kuwahusisha wadau wanaohusika na usalama barabarani katika maadhimisho hayo.

No comments:

Post a Comment