Tiketi za sherehe za kuadhimisha miaka 13 ya muziki wa Lady Jaydee zimeshaanza kuuzwa mtaani na huo hapo juu na chini ndio mfano wa jinsi zilivyo ambapo ya juu ni ile ya VIP itakayokuwezesha kupata chakula, nakala ya CD pamoja na huduma maalum ya kinywaji cha kuanzia.
Hii hapa chini ni ya kawaida itakayokuwezesha kushiriki onyesho, na kushuhudia burudani lukuki zitakazoongozwa na Profesa Jay, TID, Matonya, Grace Matata pamoja na Lady Jaydee mwenyewe na Machozi Band itaonekana jukwaani live siku hiyo.
Tiketi zinapatikaka Shear Illusions-Mlimani City, BM BarberShops-Kinondoni, City Sports Lounge-City Centre, American Nails-Kinondoni, Nyumbani Lounge-Tranic Plaza, na katika Bar za Samaki samaki
No comments:
Post a Comment