Mwanadada anayesifika kwa ku-socialize, Paris Hilton ambaye pia ni mcheza filamu mahiri, amejiunga na Busta Rhymes, Drake, Nicki Minaj, Birdman na Lil Wayne katika kuendeleza harakati za muziki chini ya Cash Money Records.
Imeripotiwa kuwa mwimbaji huyo sasa yuko 'bize' akiandaa album yake ya pili, ambayo ndani yake kutasikika sauti ya Lil Tunechi, miongoni mwa marapa wengine wa Cash Money. Album hiyo iko chini ya 'mpishi' mahiri Afrojack. Jina la album hiyo halitajwa bado.
Paris alitoa album yake ya kwanza mwaka 2006, album aliyoiita "Paris".
No comments:
Post a Comment