Ndugu, Jamaa na marafiki wa msanii Albert Mangwea wamekutana leo jioni kuanzia saa kumi jioni maeneo ya Leaders Club kuzungumzia mambo mbalimbali kuhusu msiba huo ikiwa ni kuangalia kwa pamoja kile wanachoweza kufanya kwa pamoja na taratibu nzima ikiwemo michango kuhusu msiba mzima.
Kupitia Umoja wa wao, Wasanii hao wameweza kuunda kamati ambayo inaongozwa na Mwenyekiti ambaye ni kaka wa Marehemu Kenneth Mangweha ambapo wengine waliomo katika kamati ni pamoja na Adam Juma, P Funk Majani, Mez B, Mchizi Mox, Rommy Jones, Noorah, Michelle, Lady Jay Dee, Prof Jay, J Mo, na Dj Choka ambaye atahusika na kuzungumza kupitia mitandao yani Facebook na Twitter ambapo kwa taarifa zote kutoka kwake zitakuwa zimethibitishwa na kamati hiyo.
|
Mwanamitindo Flaviana Matata, Sajjo na Mwana FA |
|
Wana kamati wakijadiliana baada ya kupewa muda wa kujadili mambo machache kabla ya kuja na taarifa yao fupi waliyoitoa kupitia kwa wadau na vyombo vya habari. |
|
Noorah, Mez B na Proffesa Jay |
|
Dada wa Marehemu Liloti Mangweha akizungumza kwa uchungu na kuelezea mengi kuhusu mdogo wake ikiwemo jinsi alivyopokea taarifa na kusema alikuwa katika hali mbaya ambayo hataisahau kwani alikuwa ndani ya daladala na hakujua kilichotokea baada ya hapo. |
|
Baba mzazi wa msanii Dully Syke akizungumza anavyomfahamu marehemu ambapo amesema atamkumbuka kuna nyimbo ilikuwa wafanye wote lakini ndio hivyo kazi ya Mungu haina makosa. |
|
Kala Jeremiah amemwelezea Ngwea kama msanii wa pekee alikuwa 100% mkali wa Free Style na alimpenda kwa nyimbo kali kama Ghetto langu iliyom inspire kuingia kwenye Game. |
|
Mwana FA amesema ni vitu vingi vya kukumbuka kutoka kwa Ngwea lakini kikubwa ni uwezo wake wa kuandika na mashairi yake kutojirudia hadi akatoa mfano kuwa mara nyingi alikuwa akimwambia Ngwea kwamba ana Range anatembea nalo kichwani lakini Ngwea alimjibu kuwa si Range moja tu bali mawili anamiliki kichwani kwake so tunaweza kuona jinsi gani alikuwa mtu muhimu kwenye game. |
|
Adam Juma alichaguliwa kama mzungumzaji wa kamati hiyo ambapo ametoa taratibu zote watakazofanya wao kama kamati ambapo amesisistza watu kushirikiana kwani msiba ni wetu sote hakuna mwenye mamlaka ya kuhodhi bali ni makubalino ya familia ndio yataendesha shughuli nzima |
|
P Funk majani nae amezungumza lakini alishindw kutokana na uchungu aliokuwa nao juu ya msiba kwani bado haamni kama Ngwea hayupo tena. |
No comments:
Post a Comment