HOME

May 22, 2013

AFRIKA YATAKIWA KUUNGANA KUDHIBITI UHALIFU WA MTANDAO!!


Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Mohamedi Gharib Bilal amezitaka nchi za Afrika kuungana kwa pamoja, kutafuta suluhisho la tatizo la uhalifu wa mitandao ambalo limeonekana kukua kwa kasi katika nchi hizo.

Makamu wa Rais amesema hayo leo jijini Dar-Es-Salaam alipokuwa akifungua mkutano wa sekta ya mawasiliano kutoka nchi mbali mbali za Afrika ukiwa na lengo la kujadili jinsi sekta hiyo inavyoweza kusaidia katika maendeleo ya nchi zao.

Makamu wa Rais amesema tatizo hilo haliwezi kutatuliwa na nchi moja, kutokana na sekta ya mawasiliano kukua, hivyo ni vema nchi hizo zikaungana na kutafuta ufumbuzi wa namna ya kulidhibiti.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania TCRA Prof: John Nkoma akizungumza katika mkutano huo amesema sekta ya mawasiliano imekuwa na changamoto kubwa ya kukua na hivyo kusababisha kujitokeza kwa changamoto zikiwemo za matumizi mabaya ya mawasiliano
Baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka nchi za Afrika, wakimsikiliza Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati alipokuwa akifungua rasmi mkutano huo wa 14 wa baraza la usimamizi wa Mawasiliano Afrika, uliofunguliwa Mei 21, 2013 kwenye Hoteli ya Double Tree jijini Dar es Salaam 

No comments:

Post a Comment