Jeshi la polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Jijini DSM leo limetoa taarifa ya kufanikiwa kuwakamata jumla ya watuhumiwa 716 kwa makosa ya kufanya biashara ya kuuza miili yao katika kipindi cha kuanzia mwezi Desemba mwaka 2012 hadi Mei mwaka huu.
Kamanda wa Polisi kanda ya Kinondoni Charles Kenyela amesema kati yao wanawake ni 678 na wanaume ni 38.
Baadhi ya watuhumiwa wa kiume waliokamatwa katika misako hiyo ni wanunuzi wa miili ya wanawake, wafanyakazi wa madanguro pamoja na wale wanaofanya vitendo vya ushoga vitendo hivyo vikiwa ni kinyume na sheria, mila na tamaduni zetu
No comments:
Post a Comment